Saturday, July 28, 2012

GAZETI A LEO




Mke wa tatu
Stori: Issa Mnally na Richard Bukos
NABII aliyesemekana ni wa Kanisa la Mashahidi wa Yehova la Kibamba, jijini Dar, Joseph Buberwa ameingia kwenye skendo ya kudaiwa kutelekeza wake zake wawili na watoto, sasa ameshatoa mahari na yupo mbioni kufunga ndoa na mwanamke mwingine wa tatu aitwaye Sarah (18).
Mke wa pili
Stori Waandishi Wetu
MLIMBWENDE mtata Bongo, Jacqueline Patrick, kama kawa, amedondosha picha nyingine chafu kwenye ‘peji’ yake ya mtandao wa BBM, Risasi Jumamosi lina ‘fulu’ data.
Jack ambaye ni mke wa mfanyabiashara Abdulatif Fundikira alitupia picha hizo Julai 25, mwaka huu huku akizisindikizia na ujumbe usemao ‘sina tatizo na mtu na mwenye macho haambiwi tazama.’
Picha hizo zimezua maswali mengi kwa watu wake wa karibu ambao wengi ni waumini wa dini ya kisilam ambao kwa mwezi huu wapo ndani ya swaumu.…

Msanii wa Filamu za kibongo, Hartmann Mbilinyi(mwenye miwani katikati) akiwa na mama yake (jina halikuweza kupatikana) wakitoka kuuaga mwili wa baba yake mlezi wa msanii huyo, Giblon Temu aliyefaliki dunia julai 23 mwaka huu katika Hospitali ya muhimbili , Dar . Mwili huo uliagwa siku ya jumatano na kusafiliswa kwenda Old Moshi, mkoani kilimanjalo kwa mazishi.

Milton Obote:


 
Apolo Milton Obote
Na Walusanga Ndaki
Rais wa Uganda aliyepinduliwa, Nyerere akampa hifadhi Tanzania

JINA lake kamili ni Apolo Milton Obote, alikuwa Rais wa Uganda tangu uhuru mwaka 1962. Mwaka 1971 alipinduliwa na mwanajeshi wa nchi hiyo, Jenerali Idi Amin wakati Obote akiwa nchini Singapore kwenye mkutano wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (Madola).

Baada ya mapinduzi hayo, Obote alikimbilia hapa Tanzania. Wakati huo rais akiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuwa rafiki yake kipenzi.

Mwaka 1980, Obote alirudishwa madarakani baada ya majeshi ya Tanzania kuuangusha utawala wa Idi Amini kufuatia vita vilivyopiganwa mwaka 1979. Alirudi madarakani baada ya upigaji kura…

John Dilinga, 'DJ JD', nae akiwaeleza wanahabari  jinsi alivyotapeliwa na Chameleone mwaka 2005.
DJ mkongwe nchini, John Dilinga Matlou ‘DJ JD’, leo nae ameweka wazi utapeli aliowahi kufanyiwa miaka saba iliyopita na mwanamuziki raia wa Uganda, mwenye hulka ya utapeli, Joseph Mayanja Chameleone.

JD, amewaeleza waandishi wa habari leo, waliokusanyika kwenye Hoteli ya The Atriums kwamba Chameleone siyo mtu mzuri anapokubaliana na mapromota, kwani hata yeye aliwahi kumtapeli dola za kimarekani 3,000, mwaka 2005.
Alisema mbele ya waandishi wa habari: “Niliwasiliana na Chameleone moja kwa moja, akanikubalia kwenye tamasha langu lililokuwa linaitwa Wakilisha. Nilimlipa dola 3,000, baada ya kupokea fedha, hakuonekana tena na hata simu yangu akawa hapoke

No comments:

Post a Comment

hey! whats up! we are happy to attend that lever we need your help by contribute with idea and other things. thank you

Featured Post

RDC-Election : élections en 2017 ou sanctions de l’UE

Comme annoncé il y a quelques jours, les ministres des Affaires Etrangères des 28 Etats membres de l’UE (Union Européenne) s...