Thursday, April 5, 2012

WEMA TENA



KAULI YA WEMA SEPETU KUHUSU DIAMOND KUKATAA KUPOKEA HELA ZAKE DIAMONDS ARE FOREVER.

Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu leo amepata nafasi ya kuzungumza na kituo kimoja cha Radio, na kuzungumza kuhusu mambo kadhaa ikiwemo sakata la juzi  kwenye show ya DIAMONDS ARE FOREVER Mlimani City Dar es salaam. Kwa kuanza Wema Sepetu amekanusha stori kwamba alikwenda nyumbani kwa kina Diamond ili amchukue waondoke pamoja kwenda Mlimani City, inadaiwa Diamond aliikataa hicho kitu kwa sababu hakutaka kujihusisha na Wema kwa vyovyote vile kwa kuwa wao sio wapenzi tena na hawajawa na ukaribu kwa kipindi kirefu. 

Sentensi nyingine ya Wema kukanusha hizo stori ni pamoja na kukiri kwamba hapafahamu nyumbani anapoishi Diamond kwa sasa, nyumba aliyokua anaifaham u ni sehemu waliyokua wanaishi wote tu. Muda mfupi baada ya Wema kuyatoa hayo maneno, Diamond alipiga simu Live na kuthibitisha kwamba ni kweli Wema alimfata nyumbani kwao siku ya show ili waende wote, hakupenda na alijiepusha kutofanya chochote ili show yake isiharibike siku hiyo, alipotoka nje akaambiwa Wema ameshaondoka.

Kuhusu ishu ya Diamond kukataa kupokea pesa ya Wema, Wema amesema “ule ni ushamba, alichofanya ni uswahili, mimi nitazidi kuwa shabiki wa Diamond, nitazidi kuwa shabiki wake na  lakini abadili tabia yake, alichofanya ni uswahili… sisi sio maadui kuna leo na kesho, nilipompelekea ile hela ni kwa sababu Naupenda sana wimbo wa mawazo sana aliokua anauperform kwa wakati huo, ndio maana alipoupiga niliamka na kwenda kumpa pesa” Alipoulizwa kama bado ana hisia za kimapenzi kwa Diamond, Wema amesema kwa sasa hana hisia zozote kwa Diamond na hayuko tayari hata kuanza ukurasa mpya wa kimapenzi na yeye. kwa kumalizia Wema amekanusha kauli ya Diamond aliyoitoa kwamba Wema anajitafutia umaarufu kupitia jina lake, kwa kusema “mimi natafuta jina kupitia jina lake, c’moooooon mimi nimekua staa since 2006 Diamond ameanza kujulikana 2007, plsss Diamond umenidisappoint…..jirekebishe” 

No comments:

Post a Comment

hey! whats up! we are happy to attend that lever we need your help by contribute with idea and other things. thank you

Featured Post

RDC-Election : élections en 2017 ou sanctions de l’UE

Comme annoncé il y a quelques jours, les ministres des Affaires Etrangères des 28 Etats membres de l’UE (Union Européenne) s...